Blogger Widgets

Tuesday, February 26, 2013

RAGE: TUTAFANYA MAAMUZI MAGUMU KWA MATOKEO HAYA

kiemba_thumb[18]
KAMATI ya utendaji ya klabu ya Simba inatarajiwa kutoa uamuzi mgumu kuhusiana na mwenendo mbaya ulionayo timu hiyo katika ligi kuu ya Vodacom.
Aidha, Rage amekanusha taarifa za kujiuzulu kwake kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo kwenye ligi hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema kwamba kamati ya utendaji ya Simba ilitarajiwa kukutana jana kwa ajili ya kujadili mustakabali wa timu yao.
Alisema kikao hicho kitajadili kwa kina hali iliyopo sasa ambayo imesabababisha timu yao kupoteza hata matumaini ya kutetea ubingwa wao.
“Tutakuna baadaye leo na kujadili hali hii maana tukiiacha hivi hivi inaweza kutuletea madhara makubwa sana…pia tutatoa maamuzi mazito baada ya kikao chetu,”alisema.
Kuhusu na taarifa za kujiuzulu kwake, Rage alisema anashangazwa na taarifa hizo zinapotoka kwani kama atafikia uamuzi huo ataitisha mkutano na waandishi wa habari na kuzungumzia hatua hiyo
…..Continue reading here: http://lindiyetu.blogspot.com/2013/02/rage-tutafanya-maamuzi-magumu-kwa.html


0 comments:

Post a Comment