Blogger Widgets

Wednesday, February 27, 2013

Madee HAKANA usanii wake soma hapa

 
Rapper wa kundi la Tip Top Connection Hamad Ally aka Madee amedai kuwa yeye sio mwana Hip Hop na wala sio shabiki wa muziki huo.
madee
Madee ambaye aliwahi kuachia wimbo uitwao Hip Hop Hailipi amefunguka kupitia Clouds FM kuwa haimbi hip hop bali ni rapper.
“Watu wanashindwa kutofautisha, mimi sio mwana hip hop mimi ni ‘rapper’ ndio maana naweza kuweka michano kwenye beat yeyote na nikafanya poa,” alisema Madee. “Nakumbuka nilipatwa na mambo mengi sana baada ya kutoa ile ngoma Hip Hop Haiuzi, sikuchukia kwa sababu nilijua kuwa waliokuwa wakinilaumu walikuwa hawajui lolote kuhusu muziki lakini walionielewa nadhani walipata picha ya kile nilichokua nikisema na kile ninachokifanya, nasisitiza mimi sio mwana hip hop na sijawahi kuwa mfuasi wa muziki huo.”

 

0 comments:

Post a Comment