Blogger Widgets

Wednesday, February 20, 2013

KAMA UNAKIU YA KUTAKA KUJUA KWANINI,KIM KARDASHIAN APEWA MILLION 800 SHOW YA MASAA 2 NIGERIA, SOMA HAPA



.
Stori za kuaminika kutoka Nigeria ni kuhusu kufahamika kwa kiasi alicholipwa TV Star wa Marekani Kim Kardashian kwa ajili ya kuhudhuria tu concert iitwayo Love like a movie february 17 2013 ambayo iliandaliwa na R&B Star Darey Art Alade, ni dola laki tano za Kimarekani ambazo kwa harakaharaka ni zaidi ya milioni 800 za kitanzania.
Unaambiwa Kim K baada tu ya kumaliza alichotakiwa kufanya, aliondoka nchini humo ndani ya saa zisizozidi 24 ambapo kwa mujibu wa Mediatakeout imefahamika baadhi ya watu waliohudhuria hiyo concert walichajiwa dola za kimarekani 640 kwa kila mmoja kupiga picha na kuparty na Kim K ambae ni baby mama wa rapper Kanye West, USD 640 ni zaidi ya milioni ya kitanzania.

Baadhi ya watu ambao wametoa maoni baada ya kuhudhuria hiyo show wamesema kumlipa Kim K dola laki 5 ni upuuzi ambao hujawahi kutokea, kisa tu ni staa huyo kutokea kwenye hiyo event na kukaa kwa muda usiozidi saa moja, staa ambae waandaaji wa shughuli walimpapatikia wakati ni mtu ambae hata Wamarekani wenyewe wanamchukia kutokana na matendo yake ikiwemo ile sex tape na mwimbaji Ray J.


.

0 comments:

Post a Comment