Blogger Widgets

Thursday, February 21, 2013

Bongo Flava, Bongo movie,Miss Tanzania,media, vyote vimechangia matokeo mabaya ya form 4, maneno ya KBC wa Kwanza Unit. Kuhusiana na matokeo mabaya ya form 4


Rapper mkongwe wa kundi linalopewa heshima kama lilitengeneza njia ya muziki wa kizazi kipya nchini, Kibacha aka KBC da Kwanzanian (wa kwanza kushoto kwenye picha) amefunguka kuhusiana na sababu anazoona zimechangia matokeo mabovu ya kidato cha nne ambayo tangu yametangazwa yamegeuka kuwa gumzo kubwa.

Kibacha amesema,  
Bongo flava+hiphop,Bongo movie,Miss Tanzania,Bongo media, kumbi za starehe,blogs,websites.. wote tunahusika kwa njia moja au nyingine kuchangia kutoa matokeo mabovu ya mitihani ya secondari 2012, ambapo 67% failed (division zero).

Hawa wanafunzi wote ni mashabiki wako!!.. lawama kubwa ya kwanza ni kwa mfumo mbovu wa elimu na uliopitwa na wakati.. “very outdated curriculum” cannot meet 21st century demands.

Wewe entertainer ndio umekuwa role model wa hawa wanafunzi, kuanzia leo nakuomba ufikirie ni jinsi gani utamsaidia shabiki wako huyo “mwanafunzi” kuzingatia masomo??

Nyie waandaji wa matamasha ya muziki, wateja wako wengi ni “wanafunzi”.. wewe mtangazaji wa kipindi maarufu katika redio na tv.. watazamaji wako wengi ni wanafunzi, kuanzia leo fikiria nini mchango wako katika kuokoa taifa la kesho.

Tusikae na kuiachia goverment na politicians, vijana hawa wanafunzi hawasikilizi siasa au bunge, wanasikiliza entertainers.. act now!! okoa jamii.

NA: http://www.bongo5.com

0 comments:

Post a Comment