Blogger Widgets

Saturday, February 23, 2013

Imamu wa Msikiti wa Mwakaje Zanzibar auawa

 

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
SIKU chache baada ya kutokea kifo cha Padri Evarist Gabriel Mushi na watu wasiojulikana kwa kupigwa risasi kichwani eneo la Beit el Raas, Jana Imamu wa Msikiti wa Mwakaje amefariki dunia baada ya kupigwa mapanga hadi kufa.

Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Khamis amethibitisha kutokea kwa tukio hilo hapo jana mchana majira ya saa 8 mchana na kumtaja aliyefariki ni Sheikh Ali Khamis ambaye ameuawa na watu wasiojulikana.

Kamanda Ahmada alisema Sheikh Khamis mbali ya kuwa ni Imamu wa Msikiti lakini pia ni mkulima na ameuliwa wakati akiwa katika mazingira ya kazi zake ndani ya shamba lake huko Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Akielezea mazingira ya tukio hilo Kamanda Ahmada alisema tukio hilo limetokea baada ya Sheikh Khamis kwenda shambani kwake katika shmba la minazi Kidoti ambapo wakati akiwa shambani hapo ndipo walipotokea watu kadhaa na kumpiga mapanga sehemu za shingoni mwake na kusababisha kifo chake muda mfupi baada ya kipigo hicho.

Alisema baada ya tukio hilo, watu walimchukua na kumkimbizwa hospitali lakini kutokana na kupoteza damu nyingi alifariki dunia wakati akiwa njiani na hivyo harakati za mazishi zinafanyika za kumzika baada ya kuchukuliwa vipimo vya wataalamu wa afya.

Kamanda Ahmada ametoa wito kwa wananchi kutopuuzia taarifa za watu ambao wanawashuku na wenye kuleta maafa yakiwemo mauaji hapa nchini, kwani kuwaficha wahalifu ni kuendeleza utamaduni usiofaa katika jamii ambayo imeanza kuharibika kutokana na mauaji hayo yanayoendelea kila kukicha.  Inna lillahi wainna ilayhi rajiiun.

0 comments:

Post a Comment