Blogger Widgets

Wednesday, February 27, 2013

HUYU HAPA YULE MSANII ALIYEMTELEKEZA MTOTO STENDI YA UBUNGO


MREMBO aliyewahi kupamba video kadhaa za wasanii wa Bongo Fleva ukiwemo wimbo wa Kidato Kimoja ulioimbwa na J.I, anayekwenda kwa jina la Maya Silemwe, amedaiwa kumtelekeza mwanaye wa kumzaa aitwaye Junior Justine (3).   Tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo mtoto huyo aliokolewa na msamaria mwema.  Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, shangazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Monalisa, alisema wao kama familia wameumizwa sana na kitendo kilichofanywa na Maya.

0 comments:

Post a Comment