Blogger Widgets

Wednesday, February 20, 2013

Diamond amenidharau mimi na amewadharau wanyarwanda wote waliokuja kumuona’ — Mico the Best

 

Unakumbuka kuna wakati Diamond Platnumz alipost picha kadhaa kwenye Blog yake akiwa anafanya Collabo na msanii kutoka Rwanda anayeitwa Mico the Best? 

Sasa Mico the Best amejikuta akiingia hasara baada ya kumlipa Diamond ambaye ameshirikishwa kwenye wimbo huo unaoitwa Sinakwibagiwe ili aende kufanya show nchini Rwanda lakini Diamond hakwenda kwenye Show hiyo.

Msanii huyo amechukulia kutotokea kwa Diamond kwenye Show hiyo ni kama dharau huku akitaka kuzungumza na Diamond ili amrudishie pesa zake ambazo alikua amemlipa in advance. 

Akiongea na vyombo mbalimbali vya Rwanda na Tanzania, Mico the Best alisema amemlipa Diamond dollar 6,000 sawa na zaidi ya Tsh milioni 9 pamoja na nauli ya ndege ya watu wanne.

“Diamond amenidharau mimi na amewadharau wanyarwanda wote waliokuja kumuona,” - Mico.

Show hiyo ilikuwa ifanyike mjini Remela, Kigali. Tunasubiri kujua ilikuaje Diamond hakutokea kwenye Show hiyo...!!!

0 comments:

Post a Comment