Blogger Widgets

Wednesday, February 27, 2013

Ray: HAYA NDIO MAJIBU ALIYOYATOA KWANINI AMEKONDA, AMEULIZA SWALI MOJA KWA MASHABIKI WAKE SOMA HAPA "Jamani siumwi bali nafanya mazoezi tu"

Muigizaji aliyepo kwenye list A ya waigizaji wa filamu Tanzania, Vincent Kigosi aka Ray ameamua kuzungumza baada ya watu kuanza kumzushia anaumwa kutokana na kupungua mwili wake kwa kiasi kikubwa.
Ray before and after

Picha hiyo ya juu inamuonesha alivyokuwa mwanzo (kushoto) na jinsi alivyo sasa (kulia).
Ray amezikanusha tetesi hizo zilizoanza kusambaa kwa haraka ambapo gazeti la udaku la Kiu wiki hii lilikuwa na habari isemayo, ‘Ray apukutika mwili’ – Kitambi chote kwishnei! Ukimuona unaweza kumpita bila kumtambua, maombi ya wakatoliki yahusishwa.
Hata hivyo Ray amesema hali hiyo imetokana na kufanya mazoezi zaidi siku za hivi karibuni. “Jamani kwani unene ndio afya au kupungua ndio ugonjwa,” ameuliza Ray.

0 comments:

Post a Comment