Blogger Widgets

Tuesday, March 26, 2013

BEBE COOL ASAFISHA HOSPITALI YA MULAGO

Bebe Cool siku ya jumapili alionekana katika hospitali ya Mulago, akisafisha kuhakikisha wagonjwa wanakaa katika mazingira safi.
mwanamziki huyo wa "kabirinage" mwanzoni alimchana Chameleon kuwa hakustahili kuwepo katika list ya wasanii matajiri Africa, ambapo Chameleon pia alimjibu kwa kusema hajali yeyote katika fikra za watu wake kuhusu utajiri wake, ila anachali yeye ni kuwapa kile wanachostahili watoto wakekutoka katika mziki wake, wakati Bebe Cool anaamini utajiri unaangaliwa katika kiasi unachokitoa kwa wanaohitaji.

siku ya jumamosi Bobi alitumia muda wake wa asubuhi kusafisha mazingira ya hospitali hiyo na mchana wake alienda kwenye uwanja wa zamani wa Rugby kuuza gari lake la kwanza na mauzo mengi kuyaelekeza katika kuchangia watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Sicle-cell nchini Uganda.

wakati houo huo siku ya jumapili ambayo itakuwa ni Easter Sunday, Bebe Cool atakuwa kwenye show ya East African Carnival inayofanyika kila mwaka akifanya show na wasanii wakubwa kutoka Kenya kama Nameless, P-Unit, Nazizi, Wyre na Uganda, Bebe Cool atasindikizwa na GNL, Rema, Mun*G, Stecia Mayanja, Sophia Nantogo na Catherine Kusasira.


0 comments:

Post a Comment