Blogger Widgets

Saturday, March 16, 2013

DIAMOND PLATINUM KUJENGA MSIKITI

 MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platinum’, amesema yuko katika mikakati ya kutafuta eneo ambalo litafaa kujenga msikiti. Diamond, aliwaahidi wapenzi wake kwamba, kutokana na kujua umuhimu wao, ameamua kuwajengea wapenzi wake msikiti ambao utakuwa kumbukumbu yake kwa watakaoutumia. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Diamond alisema ana nia ya kujenga msikiti ambao utaweka historia nzuri katika tasnia ya muziki huo. “Hata mimi nikifa leo na keshokutwa, mashabiki wangu wawe wananikumbuka kwa hilo, naamini kwa kufanya hivi hata Mwenyezi Mungu atazidi kuniwezesha kwa hili,” alisema Diamond. Diamond aliwataka mashabiki wake kumsapoti katika hilo na kuendelea kumpokea vizuri katika kazi zake, ambazo kwa kiasi kikubwa zimeliteka soko la muziki huo. Licha ya kuwa na vibao vingi ambavyo vinatamba, kwa sasa Diamond anatesa na kibao chake cha ‘Kesho’ ambacho kinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio


0 comments:

Post a Comment