Blogger Widgets

Saturday, March 16, 2013

MASTAA WAJIPANGA KWA MKESHA KUMUOMBEA KAJALA


Stori: Sifael Paul
ZIkiwa zimebaki siku 8 tu kabla ya hukumu ya staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja kusomwa Machi 25, mwaka huu, inasemekana kuwa baadhi ya mastaa wa filamu na muziki Bongo, wameandaa mkesha wa kumuombea ili hukumu hiyo iende vizuri na aachiwe huru arudi uraiani.
Kajala anakabiliwa na kesi ya kutakatisha fedha haramu kwa kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kushirikiana na mumewe, Faraji Agustino.
Kwa mujibu wa mwigizaji mmoja maarufu wa kiume, tayari ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na ujumbe kupitia mitandao ya kijamii umeanza kusambazwa kwa baadhi ya mastaa hao ambao kila mmoja anaonesha kuwa tayari kwa ishu hiyo ya kumuomba Mungu amsaidie Kajala.


Mwigizaji huyo ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alidadavua kuwa wanachotafuta kwa sasa ni mahali au nyumba ya ibada kwa ajili ya kufunga na kumwombea Kajala kuanzia saa 2:00 usiku hadi asubuhi.

“Mwanzoni ilikuwa ni kuhamasishana tu kumkumbuka Kajala katika sala zetu za kila siku kama ilivyokuwa kwa Lulu (Elizabeth Michael), lakini sasa tumeona ni vema tukakutana kwa pamoja tumlilie Mungu ili hukumu yake imuendee vizuri,” alisema mwigizaji huyo na kuongeza:

“Yah! Kajala anatia huruma sana ndiyo maana kuna wasanii ambao ni watu wa karibu yake, wapo tayari kwa ajili ya mkesha wa maombi kama (Jacqueline) Wolper, Irene Uwoya, Patcho Mwamba, JB (Steven Jacob), Ray (Vincent Kigosi), Richie (Single Mtambalike), Dude (Kulwa Kikumba) na wengine wengi.”


Katika kesi hiyo iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Kajala amesota Segerea kwa takribani mwaka mmoja ambapo sasa hatma yake itajulikana tarehe tajwa hapo juu

0 comments:

Post a Comment