Blogger Widgets

Monday, March 18, 2013

HII HAPA ILE STORI KAMILI YA MKE WA MTU ALIYEFUMANIWA AKIZINI NA SHEMEJI YAKE


MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Bahati ambaye ni mke wa Mrisho Juma, hivi karibuni alikumbwa na aibu ya aina yake baada ya kunaswa laivu ‘akingonoka’ na shemeji yake.


Tukio hilo lililoshuhudiwa na umati wa watu lilijiri Machi 11, mwaka huu mchana kweupee katika eneo la Mafisa kwa Mbambi ndani ya chumba cha Mbaji Hamis ambaye ni mdogo wa Mrisho.



Akizungumza na mwandishi wetu, Mrisho ambaye anafanya kazi ya kupiga debe katika stendi ya mabasi ya Msamvu alisema, fumanizi hilo halikutokea kwa kuweka mtego bali ni Mungu tu.


Alieleza kuwa alikamatwa Ijumaa na kutupwa mahabusu kwa kosa la kutovaa ‘yunifomu’. Mkewe na mdogo wake wakawa wanampelekea chakula.


“Jumapili jioni walikuja tena kuniletea chakula ila kwa bahati nzuri Jumatatu nikapewa onyo na kuachiwa. Cha ajabu nilipofika nyumbani nilimkuta mtoto wangu wa miaka 2 analelewa na majirani.

“Nilipowauliza mke wangu yuko wapi walidai tangu Jumamosi hajaonekana kwa maelezo kwamba amekwenda kushughulikia dhamana yangu,” alisema Mrisho na kuongeza kuwa aliendelea kumtafuta sehemu mbalimbali hadi alipoamua kwenda nyumbani kwa mdogo wake.


“Nilipofika nilimkuta mke na mdogo wangu wakiwa pamoja kitandani. Baada ya mdogo wangu kuniona alinyanyuka na kuvaa bukta kisha akatoka nduki,” alisema Mrisho.

Ikaelezwa kuwa, baada ya mwanaume huyo kumfumania mkewe huku majirani wakishuhudia, alimshushia kipigo kisha akampa talaka kabla ya kuamua kumrudisha kwao Tabora.


Akizungumza na mwandishi wetu kuhusiana na kufumaniwa huko, Bahati alisema shemeji yake alimlazimisha kulala naye baada ya kutoka polisi kumpelekea chakula mumewe.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Rehema Dimoso alikiri kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake.

SOURCE::GPL:::

0 comments:

Post a Comment