Blogger Widgets

Friday, March 22, 2013

MAMA AFANYA MAJARIBIO MATATU KUMUUA MWANAE IKIWEMO KUMZIKA HAI


mwanamke mwenye umri mdogo Adeola Joseph, aliemzika mtoto wake pekee katika nyumba yake iliyoko Osogbo kwa siku mbili  mwaka 2012, amehukumiwa kifungo cha miaka6 jela. Jaji Olusola Aluko, alitoa amri kwa mwanamke huyo mwenye  miaka 18 kifungo hicho kikiambatana na kazi ngumu, na kudai kuwa mtuhumiwa huyo ambae haonekani kutubu kwa alichokifanya, hastahili kuishi na binaadamu wengine.

mwanamke huyo ambae amethibitishwa na madaktari kuwa na akili zilizo timamu wakati wa mashtaka yake, ameishi na mtoto huyo kwa miaka 2, na ameshafanya majaribio kadhaa ya kumuua mtoto huyo anaeitwa Fatia, jaribio la kwanza lilikua November 2011 pale alipomuwekea sumu kwenye chakula, na inasemekana pia jaribio la pili lilikua december 2012 mwaka jana wakati mama huyo alipomtupa mtoto pembezoni mwa mto Osun lakini wapita njia walimuokoa mtoto huyo na kumpeleka kwenye kituo cha watoto wasio na mama ambapo baadae alirudishwa kwa mama yake.

mama huyo na mtoto waliishi pamoja mpaka pale alipofanya jaribio la tatu kumuua kwa kumzika akiwa hai, ambapo wasamaria wema walimuokoa baada ya kukaa ndani ya kaburi hilo kwa siku mbili. wananchi walimiminika kumuangalia mtoto huyo ambae amekwepa kifo kwa majaribio matatu yaliyofanywa na mama yake.
Josph aliiambia mahakama sababu zilizomfanya kufanya ukatilio huo ni ndugu zake kutokupendezwa na ndoa yake na baba wa mtoto huyo na kuamua kuishi mwenyewe bila msaada kutoka kwa mtu yoyote. Pia mshtakiwa huyo kaiambia mahakama kuwa aliamua  kumuua mtoto huyo kutokana na uamuzi wake wa kuhamia Lagos kwa ajili ya kutafuta kazi, na asinge weza kukabiliana na majukumu ya kazi na kulea mtoto.

kwa sasa mama huyu amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela na kazi ngumu.

0 comments:

Post a Comment