Blogger Widgets

Saturday, March 23, 2013

Hemed PHD "Nimeshindwa kuhandle pressure ya Wanawake Bora Nioe Sasa"



Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambae pia ni mcheza filamu hodari hapa Bongo, Hemedy PHD jana aliandika kupitia mtandao mmoja wa kijamii na kusema BORA KUOA...
Ni nini kilichomkuta PHD?? Well PHD aliandika hayo kutokana na usumbufu mkubwa anaoonekana kuupata kutoka kwa watu katika simu yake ya mkononi...
Hemedy (@hemedyPHD) ambae alilalamika kuwa amechoka na kuwa-block simu/watu hawa lakini pia kufikia kuona bora aoe alitweet " Nimeshindwa kuhandle pressure ya wasumbufu ktk simu yangu! Maisha ya kublock simu pia nimechoka! BORA KUOA! sijui itasaidia?? NABADILISHA NUMBER"

Hemedy aliandika haya huku ikonekana wanaomsumbua zaidi ni wasichana/wanawake ambapo amefikiria ni bora aoe ili kupunguza au kuondoa usumbufu huu...
Pamoja na mawazo haya, pia PHD (Star wa single GOING CRAZY) amejiuliza kama hili litasaidia kuondokana na usumbufu huu anaoupata sasa...
Hemedy amekuwa akiongelea mara kwa mara kuhusu yeye kupendwa na wasichana ambayo may be ni muonekano au kazi zake za kisanii anazofanya...
PHD pia aliwahi kusema kuwa siku akiamua kuoa inabidi aandae shindano la kutafuta mke bora (kama ilivyo katika kusaka vipaji) ambae ataishi nae milele ili kumpata yule anaefaa

0 comments:

Post a Comment