Blogger Widgets

Saturday, March 16, 2013

KING MAJUTO AGOMA KUGOMBEA TUZO ZA WAIGIZAJI MPAKA ZAWADI IWE NI TREKTA


Mchekeshaji mahiri katika tasnia ya filamu nchini, Amri Athuman 'King Majuto
MCHEKESHAJI mahiri katika tasnia ya filamu nchini, Amri Athuman 'King Majuto' ametoa mpya ya mwaka baada ya kusema kuwa si kama hapendi kushiriki mashindano ya wasanii bora bali utata unakuja katika suala nzima la zawadi.

Majuto anasema kuwa kama atatokea muandaaji na kutoa tuzo bora kwa msanii na yeye akawa mshindi basi lazima ajipangie zawadi.

Mimi umri umeenda sana na nafikiria kustaafu, najua kuna watu ambao wanasema kuwa mimi ni bora, sikatai ni kweli mimi ni bora kwa hiyo ikitokea utoaji wa tuzo na mimi nikawa muigizaji bora zawadi ninayoitaka ni trekta ili nikamalizie uzee wangu kwa kilimo bora na cha kisasa,�anasema King Majuto.

King Majuto msanii mwenye masihara kila anapozungumza na watu amesema kwamba suala la kutaka apatiwe trekta ni kweli wala hatanii kama ambavyo wengi wamemzoea

0 comments:

Post a Comment