Blogger Widgets

Saturday, March 16, 2013

Wakazi audiss wimbo wa Ney wa Mitego na Diamond ‘pumba tupu, its a cry for attention’


Wakati watu wengi wakionekana kuufurahia wimbo mpya wa Ney wa Mitego aliomshirikisha Diamond, ‘Muziki gani’ rapper wa Tanzania aishie nchini Marekani Wakazi ameudiss kwa kuuita ‘pumba tupu’.
WAKAZI PIC 2
Kupitia Twitter Wakazi ambaye anajulikana kwa uwezo wake mkubwa katika uandishi wa mashairi ya hip hop kwa Kiswahili na Kiingereza ameandika:
Wimbo wa Diamond na Ney wa Mitego ni Pumba tupu. Its a cry for attention, rather than display of Art. Shame on them!! #BongoFlavaVSHipHop. Kwanza Idea sio original, Madee na Godzilla walishafanya somethin like that.. “Hili Game”. Na Ney ha represent Hip Hop, labda Rap. And shame on whoever is goin to support huo upuuzi.
Tweet za Wakazi pia zimevuta hisia za rapper mkongwe aliyekuwa akiunda kundi la Kwanza Unit, Zavara Mponjika aka Chief Rhyson alitweet:
Kaka ndo natoka kuusikia sasa hivi nlidhani ni wa mda mrefu ulinipita. Inachekesha sana, watu wanadhani ukirap tu basi ndo’ Hiphop. Ni kweli hizo ni juhudi za walio nyuma ya pazia sio yeye mwenyewe. Jamaa wanaona vuguvugu la fani hii linaimarika sasa WANATAHARUKI.
Zavara (kushoto) akiwa na Ruge
Zavara (kushoto) akiwa na Ruge
Zavara ameongeza, “Jamaa hawezi kuwa MC na akubali kuchana kwenye mdundo dhaifu wa Bongofleva na aanze kuitetea fani ambayo yeye hayumo. Tuipotezee tu.”
Wakazi pia aliongeza kwa kumjibu Zavara, “kaka ni wakati kila jiwe lifunuliwe. Hatuwezi kuwa misrepresented alafu tukae kimya. Na jamaa inabidi ifunguke macho ili kuendelee.Mi na wa target hao artists, maana they have antiques za kutumia migongo ya watu, to get shock value!! Listen to their words.”
“Nakubali kaka, sasa basi kama hivyo umeamsha mzuka wangu wa kimapinduzi sasa. Mi namkubali sana Diamond ka mwimbaji, anakosa dira tu,” amefunguka Zavara. Huyo Ney, sijawahimsikia kazi zake ila jina nshasikia. Uzuri najua we’haichukui muda kunyonga jiwe fulani ITAPOBIDI..ibwagie mapande.”
“Hata mi namkubali Diamond as a singer, inasikitisha tu anavyoegemea kwenye shock value wakati ana uwezo artistically. #NameDroppin. Hiyo Kazi nampa Nikki Mbishi. Mi nipo na fight Tanzania tupate respect kimataifa,”amemalizia Wakazi.

0 comments:

Post a Comment