Blogger Widgets

Thursday, March 14, 2013

KWELI HII SASA NI SODOMA NA GOMORA BABU WA MIAKA 70 AFUMANIWA AKIWA NA MKE WA MPANGAJI WAKE

                                  


SIKU chache zilizopita, gazeti moja  maarufu  hapa  nchini liliripoti juu ya fumanizi la babu mwenye umri wa miaka 70, Rafael Mitasio aliyenaswa gesti akiwa na mke wa mpangaji wake. Taarifa tulizozinasa zinadai kuwa mzee huyo amesusiwa mwanamke huyo.

Chanzo chetu cha habari kimedai kuwa, mara baada ya habari hiyo kutoka gazetini, mume wa mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina lababa Tausi aliumia sana.

“Ile habari ilipotoka kwa kweli mume wa yule mwanamke aliumia sana, akaamua heri huyo mzee amchukue kabisa kama ameona anaweza kumtunza kuliko yeye. 
            
“Cha kushangaza yule mzee naye eti anadai wala habari hiyo haijamuumiza na anasema atamuoa kabisa mwanamke huyo ili kuwakata vilimilimi wabaya wake,”kilidai chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Mzee Rafael alipotafutwa kuzungumzia kama kweli ana mpango wa ‘kumchukua jumla’ mwanamke aliyenaswa naye wakivunja amri ya sita, alizungukazunguka sana lakini mwisho akasema:

‘’Si mmeshaandika kuwa nimefumaniwa, haya kaandikeni tena kuwa nataka kumuoa kabisa ili mfurahi.”
Hata hivyo, fumanizi hilo lilizua kizaazaa cha aina yake hadi likafikishwa polisi.

Hii story Nimeitoa huko sweethome1.blogspot.com, nimeona nishee hapa maana nikituko, babu wa 70 bado anadai lol hapana chezeya mambo flani yaleeee, unaambiwa eji iz nasingi bati e namba lol kafurahiaje alivyosusiwa my wife wake hahahaha

0 comments:

Post a Comment