Blogger Widgets

Monday, February 11, 2013

Baba Mtakatifu, Papa Benedict XVI atangaza kuachia madaraka tarehe 28 Februari: SOMA STORI HII HAPA



Baba Mtakatifu, Papa Benedict XVI KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani,

Papa Benedict XVI ametangaza kuachia madaraka ya kuongoza kanisa ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, uamuzi ambao ni wa kwanza tangu karne ya 15 kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Habari la AFP. 
Katika taarifa yake, Papa amesema amefikia uamuzi huo ambapo sasa ana umri wa miaka 85.Msemaji wa Papa, Federico Lombardi amesema kiongozi huyo wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki duniani, ataachia ofisi rasmi tarehe 28 Februari, mwaka huu saa mbili kamili asubuhi. 
Wachambuzi mbalimbali wa masuala ya Vatican wanasema safari hii, kuna uwezekano mikoba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI ikarithiwa na Kardinali kutoka Afrika. Kardinali Peter Turkson wa Ghana ametajwa kama mrithi-mtarajiwa wa nafasi hii nyeti ndani ya Kanisa Katoliki, linalokadiriwa kuwa na waumini zaidi ya bilioni moja dunia nzima. Mwingine ni Kardinali Francis Arinze; mzaliwa wa Nigeria ambaye alichukua nafasi ya Benedict XVIkama Kardinali-Askofu wa Velletri-Segni alipoteuliwa kuwa Papa miaka nane iliyopita.

0 comments:

Post a Comment