Blogger Widgets

Saturday, February 16, 2013

Picha ya rais Hugo Chaves wa Venezuela zatolewa hadharani tangu alipoanza kuugua. ANGALIA HAPA



Picha na NYDailynews.com
Serikali ya Venezuela imetoa hadharini kwa mara ya kwanza picha za rais Hugo Chaves ambae hajaonekana katika macho ya umma wa taifa hilo tangu Desemba mwaka jana.
Katika picha hizo rais Chaves anaonekana amelala kitandani huku  Mabinti wake wawili wanaonekana wakiwa wamesimama pembezoni mwake.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 58 anaendelea kurejea katika afya yake baada ya kupata matatizo yanayohusishwa na upasuaji wa ugonjwa wa saratani.
Mpaka sasa serikali ya Venezuela anaendelea kumsubiri Chaves apate nafuu ili aweze kuapishwa ili kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine wa miaka sita.

0 comments:

Post a Comment