Blogger Widgets

Sunday, March 10, 2013

FREEMASONS WANAVYOJIHUSISHA NA NAMBA 666


Katika kuhakikisha kwamba serikali moja ya dunia inaanzishwa, freemasons walianzisha vitengo mbalimbali kwa madhumuni ya kufanikisha lengo lao. Ndipo kikaundwa chombo kinachoitwa ‘Trilateral Commission’ kinachounganisha nchi za Marekani (jimbo namba 1), Ulaya (Jimbo namba 2) na Japan (jimbo namba 3). David Rockefeller ndiye aliyeanzisha chombo hiki na kubuni nembo inayotambulisha chombo hiki ikiwa ni namba 666. Katika picha ya nembo ya trilateral commission,  utaona upande wa kushoto mishale mitatu iliyopinda na kuunda mfano wa mduara. Hiyo ndiyo nembo ya Trilateral Commission. Unapoichunguza kwa makini nembo hiyo utagundua kwamba kuna mishale mitatu iliyopangwa kwa pamoja huku kila mshale ukitengeneza namba 6 na hivyo kuunda mishale mitatu yenye namba 666

Nembo ya Trilateral commission.
Wakati waprotestant wamekuwa wakipinga muungano wa serikali na dini pamoja na mafundisho machafu yaliyochanganya ukweli na uongo, wamekuwepo viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa wakipinga vikali mipango ya freemason katika kuundwa kwa serikali moja itakayotawaliwa na watu wachache. Ingawa baadhi ya viongozi wa kisiasa ni wanachama wa freemasons, hata hivyo wengi wao wamekuwa wakipinga mipango ya freemason inayoonekana wazi kuugawa ulimwengu katika makundi ya wenyenacho na wasionacho. Alikuwepo rais Muammar Gadhafi ambaye alipinga vikali mipango ya familia ya Rothschild kutaka kutawala sekta ya fedha duniani kote.

0 comments:

Post a Comment