Blogger Widgets

Wednesday, March 13, 2013

HIVI UNAJUA ALIYETUPIA PICHA ZA UCHI ZA AGNESS NI NANI? HUYU HAPA

                                                                            AGNESS.


Mrembo 'Classic'  Agness Gerald 'Aggy Masogange' anayeng'arisha nyota yake kupitia video za wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, amemtupia zigo la lawama mwigizaji Christina Manongi 'Sintah' kufuatia kuvuja kwa mkanda wa video unaomuonyesha akiwa mtupu.

Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo kimoja cha redio Bongo, Aggy, amefunguka kuwa akiwa safarini nje ya Bongo alipewa taaraifa za kupotea kwa Digital Camera ambayo anadai ndiyo ilitumika kurekodia video hiyo na baada ya uchunguzi kufanywa na watu wake wa karibu iligundulika kuwa mwigizaji huyo ndiye anahusika na kupotea kwa kamera hiyo huku pia akidai ndiye aliyefanya kazi ya kusambaza video hiyo kwenye vyombo vya habari na mitandao kadhaa.

"Nilipewa taarifa ya kupotea kwa kamera hiyo, nina hakika atakuwa SINTA ndiye aliyefanya kazi ya  kuisambaza, awali nilitaka kuchukua hatua juu ya jambo hilo lakini nikashauriwa na watu wangu wangu kuwa nisifanye hivyo, kwa kweli najisikia vibaya lakini namwachia Mungu”. Alisema.

1 comment:

  1. Unamuachia mungu EEeeeeee!!!!!! na wewew ulivyokuwa unapiga picha hizo unalikuwa unategemea nini!!!?

    ReplyDelete