Blogger Widgets

Monday, March 4, 2013

Huyu hapa yule Mbunge aliyekutwa akifanya tendo la ngono na wanawake wawili.

  Huenda mliwahi kusikia mkasa uliompata mmojawapo wa viongozi wa ngazi za juu kabisa katika serikali ya nchi ya Liberia iliyoko huko Afrika Magharibi.

Huyu ndo ndo Bwana Mkubwa Willie Knuckles aliyekuwa waziri wa mambo ya rais(Minister of Presidential Affairs) huko Liberia ambaye alilazimika kujiuzulu baada ya picha zake zilizokuwa zikimwonyesha akifanya tendo la ngono na wanawake wawili kusambazwa kwenye mtandao.
Kwakweli bado haijaeleweka hasa walioamua kumsambaza mtandaoni walikuwa na lengo gani naye zaidi ya kumdharirisha na kumfedhehesha namna hii.
Ilikuwa ni aibu kubwa sana kwake na kwa familia yake,serikali ambayo yeye alikuwa ni mhimili wake na hata wananchi wote wa Liberia (picha hii nimekata "croping" makusudi kulinda maadili ya mtanzania,lakini shughuli iliyokuwa inafanyika nafikiri inaonekana).
Haijaelezwa vizuri kuwa ndoa yake ambayo ilikuwa na takribani miaka 37 mpaka anakutwa na maswahibu haya iliishilia vipi,vyovyote ilivyokuwa Bwana mkubwa Knucles atakuwa alivuna alichokuwa amekipanda.
Hapa Tanzania kina" Willie Knucles" wako wengi sana,wababa wanaopenda kutumia nyadhifa zao na mapesa yao ambayo kwao huona ni vijisenti kwa kuwarubuni mabinti tena wadogowadogo na kufanya nao ngono.
Binafsi huwa nashikwa na hasira sana ninapoona binti mdogo anatoka na M'baba anayefaa kuwa Baba yake Mzazi ni mambo ambayo yapo sana katika jamii yetu hata kijijini kwangu ninapoishi Kiluvya wazee wa type hii wapo sana ndo maana kasi ya kusambaa kwa virusi hatari vya Ukimwi inazidi kukua kila kukicha,in which way tunaweza kupona ikiwa mambo haya yataachiwa yaendelee ku'apply katika jamii zetu?
Lakini na nyie ma'binti hivi na lazima kweli m'date na Wababa wanaolingana na Wazazi wenu?(hili nalo ni swali ninaloliulizaga sana... majibu ambayo nimekuwa nikiyapata yamekuwa hayaniridhishi hata kidogo,eti utamsikia demu anasema eti Vijana wasumbufu sana....nyie mmelogwa?)
Blog hii inatoa tahadhari,yaliyompata Bwana Willie Knucles iwe ni fundisho kwa wote wenye tabia hii,siku hizi technolojia imekua sana,unaweza kudhalilishwa dunia nzima katika dakika chache tu,kuna simu za kichina siku hizi zina Camera 4,4 (mbele nyuma na pande zote 2)
Shauri zenu mnaweza kujikuta kwenye "The World of Anselm" mkabaki kunisaka kwa udi na uvumba.

chanzo:hans4real.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment