Blogger Widgets

Sunday, March 3, 2013

MASHAIRI YA YOUNG KILLER - DEAR GAMBE.




VERS 1;
Dear gambe umefanya maisha
yangu ya yumbe,
MI nimpambe wako leo
nimekutumia ujumbe,
MI ndugu yako nipe ukweli
usini fumbe,
Uwepo wako karibu vp
unafanya ni yumbe,
Kila muda kwene friji
unajipoza,
MI domo zege nikisha kutumia
natongoza,
Nalewa usiku kucha jua lina
chomoza,
Nasindikiza na supu asuhi
njema unaniongoza,
We ni nani unaiyendesha hi
akili,
Nnikiwa na mawazo unanitoa
stress nisifikili,
Ukiwa mezan chupa kadhaa
sijiwezi,
Mpaka mtaani washa nipa jina
jingine la mlevi,
Unafanya nafubaa mi
mwenzako,
Hadi kazini naiba chapaa nije
kwako,
Dear gambe mitaa ipe ukweli
wako,
Nakila ugomvi wa baa kwanini
chanzo ni chako.. 


VERS 2;
Unafanya ndoa nyingi
zinavunjika,
Hasi chanya we na msosi
nikichanganya na tapika,
Aukatai kila mteja anae
kuarika,
Unafurahi na ubaridi wa maji
una chilizika,
Likitokea tatizo we ndo
kimbilio,
Nakutinga nakua muongeaji
bila mpangilio,
Nasahau kinga tamaa ndo
kimbilio,
We ni funda la ziada
unaniumbua mi mwenzio,
Unarainisha koo kifikla unani
bembeleza,
Unani kontro sijasoma
naongea hadi kingereza,
Usha niweza nani aliye
kutengeneza,
Na nini aliwaza nawe ni
mbaya kwa wasio jiweza,
Sa najinyea nanilikunywa kwa
furaha,
Najikojolea unani athiri na
ninatoa cha paa,
Dear gambe mitaa ipe ukweli
wako,
Nakila ugomvi wa baa kwanini
chanzo ni chako.. 


VERS 3;
Dear gambe unanichanganya
sana,
Unamajina mengi mpaka ya
mbuga za wanyama,
Nashangaa,mengine yanatia
kinyaa,
Mfano mzuri nigongo
chimpumu hata cha ng"aa,
Kwenye ubongo umetawala
kila secta,
Niukweri siwezi kua nawe bila
pesa,
Watu wengine wana kula ada
kisa wewe.
Unawafanya wanasahau
ibada,
Na juzi juzi tu nimepata
khabari,
Kuna mwana ulikua nae
ameshapata ajaLI,
Dear gambe nikweli
unanichosha,
Napenda kua nawe ila
nyumbani mboga wanakosa,
Nawaza jinsi gani ntakuacha,
Mpaka wazalendo wa dini
bahadhi kwako wame data,\
Hakuna utata poa sasa
najikata,
Kapuku nikizipata ntakufata...

0 comments:

Post a Comment