Blogger Widgets

Monday, February 4, 2013

HIZI HAPA VURUGU KATI YA CHADEMA NA CCM HAPO JANA BAADA YA KUGOMBANIA ENEO LA KUTUNDIKA BENDERA ZAO

 
Wafuasi wa CCM wakimtoa nduki mfuasi wa CHADEMA, Arnold Swai, wakati wa vurugu zilizotokea eneo la Mwanga Baa, mkoani Dodoma jana wakati CCM wakifanya mkutano ambao ni sehemu ya sherehe za miaka 36 ya kuzaliwa kwake.

 
 Wafuasi wa CCM na wafuasi wa CHADEMA wakigombania mti ambao ulikuwa unatakiwa kupandisha bendera
 

Mbunge wa Tabora Mjini(CCM) Ismail Aden Rage(wa pili Kulia aliyeshika bomba) akipambana na vijana wa chadema eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.
Kada wa Chadema Mkoani Dodoma, Arnold Swai akipokonywa mti wa bendera ya chadema na wafuasi wa CCM jana, baada ya kutokea vurugu katika eneo la Mwanga baa, Dodoma 

Mfuasi wa CHADEMA akikimbiakipigo alichoangushiwa na wafuasi wa CCM eneo la uwanja wa wazi karibu na  Mwanga baa, mkoani Dodoma sehemu ambayo CCM walikuwa wanaadhimisha miaka 36 ya kazaliwa kwa chama hicho kata ya Uhuru, ambapo CHADEMA walikwenda kuweka bendera yao sehemu hiyo
Mmoja wa wafuasi wa CHADEMA waliokamtwa katika sekeseke hilo akiwa ndani ya gari la polisi
Wafuasi wa CCM Wakimnyang'anya bendera ya CHADEMA mfuasi wa chama hicho aliyetaka kuiweka bendera hiyo sehemu ambayo ilikuwa inafanyikia maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM kata ya Uhuru mkoani Dodoma.
 
Mmoja wa Wafuasi wa Chadema akishikwa na polisi baada ya wafuasi wa CCM na Chadema Kugombea eneo na mti wa kutundika bendera za vyama vyao.
Picha Zote na Mpoki Bukuku

0 comments:

Post a Comment