Blogger Widgets

Sunday, February 3, 2013

SIRI NZITO ZA JACKLINE WOLPER ZAVUJA

Actress Jackline Wolper amefichua siri nzito ya urembo wake kwa kitu kinachomfanya aendelee kuonekana kuwa mrembo na kubaki na mvuto wake wa asili Akizungumza na theHOODunfotainment Wolper alijikuta akiweka wazi anachokifanya ili kuendelea kubaki na urembo wake huo huku akisisitiza kuwa mazoezi ya viungo vya mwili na kutokunywa bia ni siri kubwa ya urembo wake Wolper hakusita kuweka wazi kuwa yeye ni mtu wa kula mbogamboga,samaki, maziwa na matunda kwa wingi huku akipata muda wa kupumzika ili kujenga mwili wake bila ya kusahau kunywa maji kwa wingi kwani hayo yanamfanya ngozi yake iendelee kuwa yenye mvuto Wolper alisisitiza kuwa katika maisha yake hutumia kula nyama nyeupe na kuepuka nyama nyekundu ili aendelee kubaki hivyo alivyo kuepuka kuwa mnene na kutoka kitambi kama baadhi ya wanawake wengine wanavyokuwa 
 
 

0 comments:

Post a Comment