Blogger Widgets

Friday, March 1, 2013

Hemedy asema Jaji Ian wa Tusker Project Fame ndiye aliyesababisha awe alivyo leo

page

Katika shindano la Tusker Project Fame season 2, Hemedy Suleiman na Jaji Ian Mbugua hawakuwa wakipikika kwenye chungu kimoja. Ian hakuwahi kumkubali muimbaji huyo aliyegeuka kuwa muigizaji wa filamu pamoja na kujitahidi kuchagua nyimbo zinazoendana na sauti yake.
Na hata katika shindano la Tusker AllStars mwaka 2011 ambapo Hemedy alishiriki pia, mafahari hao hawakuiva pamoja. Baada ya kuchoshwa na maneno ya kukatisha tamaa ya Ian Hemedy, PHD alienda mbali zaidi kwa kutoa kauli, “Ian first of all you are not hot like me and secondly you don’t have a movie or a single to your name,” Hemedy alimuambia Ian ambaye hata hivyo akibaki kucheka tu.
Lakini leo hii, Hemedy amekiri kuwa, Ian ana mchango mkubwa katika mafanikio yake baada ya kumwambia kupitia Twitter, “shout outs to judge @IanMbugua for pushing me to get here!!You were my HERO but in your own way!!…..LOOK AT ME NOW!!HERE I STAND#BIG STAR.”
Wakati mwingine waswahili husema akuambiaye ukweli anakupenda

0 comments:

Post a Comment