Blogger Widgets

Wednesday, March 6, 2013

HII HAPA TAARIFA KAMILI KUHUSU TUKIO LA KUMUENZI STEVEN CHARLES KANUMBA



WASANII wa filamu Tanzania wapo katika harakati za mwisho wa mchakato wao katika maandalizi ya kumuenzi marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni moja ya jambo walilokusudia kuhakikisha wanamuenzi na kuthamini mchango aliouacha kwenye tasnia ya filamu

Akizungumzia maandalizi hayo jijini Dar es Salaam rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifwamba alisema kuwa baadhi ya maandalizi yameanza kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba, huku wakishirikiana na familia ya marehemu ili kuweka mipango ya nini kifanyike katika harakati za kutimiza lengo
Alisema kuwa lengo lao lazima litimie kwa sababu walikusudia kufanya kitu kwa ajili ya kumuenzi marehemu kutokana na mchango wake aliouacha kwenye filamu na ili kudhihirisha hilo wanaamua kumenzi katika hali ya kiupekee
"Lazima tufanye kitu cha tofauti katika kumuenzi marehemu na ili tuonyeshe upendo wetu lazima tuheshimu kile alichokiacha kwa kuendeleza" alisema Mwakifwamba
Aliongozea kuwa muda ukifika na maazimio yakipitishwa ndipo ataweka wazi ni jambo gani lililokusudiwa kufanyika
Marehemu Steven Kanumba amefariki april 7 mwaka 2012 ambapo chanzo cha kifo chake kinadaiwa kuwa ni ugomvi wa mapenzi, na aliyekuwa mpenzi wake msanii mwenzie wa filamu  Lulu

0 comments:

Post a Comment