Blogger Widgets

Monday, March 11, 2013

HII SASA NI ZAIDI YA LAANA..... WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARY TANZANIA NAWAO WEMEPIGA PICHA ZA UTUPU


Wakati  mwingine nikifikiria  huwa  naumia sana.Siku  zote najiuliza  ni kitu gani kimetufikisha hapa tulipo? Ni  tamaa, ulimbukeni au  ndo umaskini unatutesa?.

Najaribu kuangalia mbali  lakini sioni tumaini  lolote.  Naona tumetandwa na giza nene na hatujui nini cha kufanya.....

Kama utakumbuka, tumewahi kuripoti  juu ya sakata la  POLISI WA KIKE KUPIGA PICHA AKIWA UCHI.  

Hatukuishia hapo, tuli ripoti tena juu ya sakata la KIGOGO  WA SERIKALI (MKE WA MTU ) KUFUMWA GESTI NA MUME  WA MTU........
 Nakumbuka  pia tumewahi kuripoti juu ya sakata la MZEE MMOJA ALIYEFUMWA  GESTI NA MWANAFUNZI....

Bado tuliendelea kuripoti  juu ya sakata la  WANAFUNZI WA CHUO KIKUU  WALIOJIREKODI WAKIFANYA UCHAFU   NA WENGINE AMBAO WALIAMUA KUJIUZA......

Kama haitoshi, bado tuliendelea kuripoti juu ya UCHAFU  MBALI  MBALI  WA WASANII WA HAPA NCHINI  ambao wamekuwa  wakipiga picha chafu na kuziachia   mitandaoni..

Leo hii hadi wanafunzi wa sekondari nao wameiga???.....Nani alaumiwe? Askari ambaye pengine  anajukumu la kulinda sheria naye anapiga picha chafu.

Mzazi ambaye ni mlezi  anaamua kutembea na mwanafunzi,tena wa kidato cha pili........

Ndugu zangu, japo ni mambo ya kawaida kwa wengine, lakini ukweli ni kwamba hali  inatisha sasa. Hali ni mbaya jamani.

Huyu   ni mwanafunzi ambaye ni nguvu kazi ya taifa. Hili  ni taifa gani tunaloliandaa?.....

Unamaoni  gani  msomaji wetu   ambayo pengine yatasaidia  kurejesha heshima yetu?
FROM-MPEKUZI

0 comments:

Post a Comment