Blogger Widgets

Thursday, March 7, 2013

UNAIFAHAM KAULI YA UEFA KUHUSU REFA ALIEMPA LUIS NANI KADI NYEKUNDU MARCH 5? IKO HAPA

.
.
Taarifa ikufikie kwamba UEFA wamesema hawana tatizo lolote na kadi nyekundu iliyotolewa kwa mchezaji wa Man U Luis Nani kwenye mechi na Real Madrid March 5 2013.

UEFA wamesema hawana tatizo lolote na uamuzi wa refa Cuneyt Cakir kutoa hiyo kadi na vilevile refa huyo ataendelea kuwepo kwenye list ya marefa wanaohusika na UEFA.

Pamoja na kusema hayo, UEFA imesema inasubiri official report ya mechi yenyewe ili kujua kitakachoripotiwa lakini kumbuka kwamba Cakir Cakir ambae anatarajiwa kuchezesha kwenye kombe la dunia 2014, sio mchoyo wala mzito wa kutoa kadi nyekundu… mwaka jana kwenye semi-final alimpa kadi nyekundu John Terry wakati Chelsea ilipocheza na Barcelona.

Pamoja na kwamba UEFA hawana noma na kadi hiyo nyekundu, wachezaji hawa wanne ni miongoni mwa waliopaza sauti kuikataa hiyo kadi, yani waliipinga waziwazi kabisa kama unavyoona tweets zao.

0 comments:

Post a Comment