Blogger Widgets

Tuesday, March 12, 2013

WEUSI WAANZAISHA HARAKATI ZAO WENYEWE BAADA YA UMOJA WA WASANII KUSITISHA MIKATABA NA MAKAMPUNI YA RINGTONES KUPOTELEA NJIANI

 
Baada ya wasanii na uongozi wao uliokuwa ukipigia kelele maswala ya makampuni ya simu na yale yanayouza ring back tones na call back tones (Push Mobile na Spice) , kutokueleweka, na kutokujulikana harakati hizo zimeishia wapi, leo hii muwakilishi wa Weusi, Nikki wa II ametangaza kujitoa katika umoja huo na kuamua kuandika barua yao kama Nikki na Joe na ofcourse kama Nako 2 nako pia, tayari kwa ajili ya kupeleka katika makampuni hayo

"mimi na Joe Makini tumeshakamilisha barua yetu na tumeshaiwakilisha push mobile na spice, barua ya Noko 2 nako ipo on progress nadhani leo jioni kesho tunaipeleka, kwasababu ile biasha kwa upande wetu tumeona haina maslahi, hailipi, kwasababu ukiangalia mkampuni ya simu yanachukua asilimia 70 ya kile ambacho kinapatikana, halafu 30% ndio inaenda kwenye ile kampuni ya ring tone, na kile ambacho kinaenda kwenye ile kampuni ya ringtone almost  ile kampuni inachukua 90%,"

 "kwahiyo we msanii unaambulia asilimia 10 mpaka 6 wakati mwingine, hiyo ni moja pili ni kwamba hauwezi hauna namba ambayo unaweza kujua ni watu wangapi wamenunua mziki wako au wamedownload rigtone yako, kwamfano mimi nyimbo yangu ya haya na good boy ambazo zimeuza na kampuni ya push mobile, kwanza good boy ndio nilisaini nao haya sikusaini nao waliuza bila makubaliano, nikaenda kuulizia malipo yangu ya miaka miwili ya nyimbo zanu ya good boy na haya kwa miaka miwili walinipa shilingi 60,000 ya Tanzania, kwahiyo yaani hii ni biashara inayowanufaisha makampuni ya simu na watu wa Ringtones..........."

Nikki aliedelea kusema "bidhaa sio ya kwao wao wamepanga bei wanavyotaka, na ndio biashara inavyofanyika hivyo, ni biashara ya kinyonyaji."

kama unakumbuka vizuri mwaka jana mwishoni kulikuwa na umoja wa wasanii ambao waliamua kujitoa na kusitisha mikataba yao na kampuni hizo mbili na Weusi pia wakiwemo ndani, ila sasa Weusi wameamua kufanya haakati hizi na kuandika barua kama wao, sababu hasa za kufanya hizo Nikki amezielezea

" sisi kama weusi pia tumesikitishwa na namna ambavyo viongozi wa ile movement, walivyoongoza harakati zenyewe, kwamfano wasanii tulitafutwa tukajioganaiz, tuksaini zile pepa za kwamba turidhia kuwa mikataba yetu ivunjwe, na watu wakaenda kwenye media wakasema kwamba kuna hichi kitu na wanaki push foward, lakini kumbe hawa watu walikuja kupanga kikao cha kuja kuonana na watu wa makampuni ya simu, kwahiyo maana ya kuwa ni wawakilishi, wangetakiwa kurudi kwa wasanii wakatuambia jamani eeh, si siku flani tunakikao na hawa jamaa, kwa hiyo sisi kama wasanii tungewaambia tunataka muongee moja mbili, tatu nne tano, wangeenda kutuwakilisha, hawakufanya hivyo,umeona, wakaenda kuongea wenyewe wanajua walichoenda kuongea, baada ya kuongea hawakurudi kutupa feed back, kwamba tumeongea na jamaa tumewaambia hivi, tumefikia hivi, hawakurudi kutuambia."

"mi nilimskia tu Mwana Fa juzi katika interview, tena hilo swali aliulizwa bahati mbaya tu, injamaana asingeulizwa hilo swali, asingetoa ile feedback, kwahiyo nini sasa dhani ya wale kuongoza ile movement? walienda kuongoza mawazo ya wasanii, kwahiyo kikao chao walichafanya na watu wa push na spice wangetakiwa watuambie, wakachukua mawazo yetu na wakatupa feed back, lakini imepotelea hapo katikati, hatuwezi kujua yaani ni nini. kwahiyo hata sisi tulioamua kuingia kwenye hiyo movement tumekuja kuonekana hatuna maana, sababu tulipiga kelele nyingi kwenye media halafu tukapotea ghafla.."

0 comments:

Post a Comment